Kulingana na talkSPORT, mazungumzo kati ya Chelsea na Mauricio Pochettino yanaendelea
Meneja huyo wa zamani wa Tottenham sasa ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba huko Stamford Bridge baada ya mpango wa Luis Enrique na Julian Nagelsmann kushindikana
Uamuzi unaweza kufanywa katika siku zijazo huku uongozi wa Chelsea ukitarajia kumtangza kuwa meneja wao kuanzia msimu ujao
Kwa sasa Chelsea inanolewa na kocha wa muda Frank Lampard ambaye tangu akabidhiwe mikoba, imekuwa sio rahisi kwake kupata ushindi