Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano April 26 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Apr 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano April 26 2023

Liverpool wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips msimu wa joto na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 yuko tayari kuhama. (Star)

Chelsea watafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan, na watamuuliza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kama anataka kufufua soka lake la Blues chini ya mkufunzi mtarajiwa Mauricio Pochettino. (Telegraph - usajili unahitajika)

Kocha wa muda wa Chelsea, Frank Lampard yuko tayari kuzungumza na Pochettino kuhusu kikosi cha The Blues ili kusaidia mabadiliko yanayotarajiwa ya Muargentina huyo kuwa rahisi iwezekanavyo. (Evening Standard)

Tottenham, Chelsea na Manchester United wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 27, msimu huu. (Football Insider)

Chelsea wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Cameroon Andre Onana, 27, kutoka Inter Milan na wanaweza kumtumia kipa wao wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 28, kama sehemu ya mkataba huo. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Ryan Gravenberch, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool, anasema anataka kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza katika klabu ya Bayern Munich msimu ujao na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atasubiri kuona kitakachotokea katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Voetbal International - kwa Kiholanzi)

Kocha wa Newcastle United Eddie Howe atakuwa na bajeti ya uhamisho ya hadi pauni milioni 150 kutumia msimu huu wa joto. (Sun)

Newcastle wanamfuatilia beki wa kati wa Roma na Brazil Roger Ibanez, 24. (Nicolo Schira)

Newcastle inatafakari uwezekano wa kumuuza winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, 26, msimu huu wa joto. (Football Insider)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’