Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, lakini hawako tayari kuhusika katika mvutano wa muda mrefu kuhusu ada ya uhamisho wake na Tottenham.
United wana nia ya kumsajili mlinda lango wa Dinamo Zagreb kutoka Croatia Dominik Livakovic, 28, huku mkataba wake na kipa wao David de Gea ukimalizika msimu huu. (Jutarnji, kupitia Football 365)
Mauricio Pochettino hamtumii wakala wakati anapojadiliana kuhusu kuteuliwa kwake kama kocha mkuu mtarajiwa wa Chelsea. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kipa wa Uhispania David Raya na mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, wote 27, wanafuatiliwa na Chelsea kwa ajili ya uhamisho wa majira ya joto kutoka Brentford. (Football London)
Chelsea wanatazamiwa kukutana na Inter Milan kujadili mustakabali wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Serie A, pamoja na uwezekano wa kumsajili mlinda lango wa Cameroon Andre Onana, 27. (Evening Standard )
Liverpool wanaweza kutumia pesa nyingi kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan na Italia Nicolo Barella, 26, licha ya kukataa kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, msimu huu kwa sababu ya bei ya juu ya Borussia Dortmund. (Sport Mediaset kupitia Express)
Vilabu vya Arsenal, Tottenham na Newcastle vinavutiwa na mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 26, ambaye Barcelona wanaweza kumuuza ili kupata pesa za kumnunua tena mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, kutoka Paris St-Germain. (AS - kwa Kihispania)
Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Emile Smith Rowe, 22, ambaye "ametamaushwa" na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha The Gunners. (Football 365) Mshambulizi wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, amekataa ofa za kujiunga na Real Madrid na Chelsea. (La Gazetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
BBC