Maafisa wa Real Madrid watasafiri hadi Ujerumani wiki hii katika jitihada za kumshawishi kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 19, kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania msimu huu wa joto. (Marca kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24, yuko kileleni mwa orodha ya wachezaji wanaolengwa na Arsenal msimu huu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa Manchester United na Brazil Casemiro, 31, ananyatiwa na Thomas Tuchel katika klabu ya Bayern Munich msimu wa joto. (Kicker - kwa Kijerumani)
Mkufunzi wa Bayern Thomas Tuchel pia anataka kuungana tena na kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic, 28. (Sport1 - kwa Kijerumani)
Bayern, hata hivyo, hawana nia ya kumuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Ryan Gravenberch mwenye umri wa miaka 20 msimu huu, licha ya vilabu vya Liverpool, Manchester United na Arsenal kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (CaughtOffside)
Mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsmann yuko kileleni mwa orodha ya wachezaji wanne walioteuliwa kuwa mkufunzi mtarajiwa wa Tottenham Hotspur lakini Mjerumani huyo, 35, anaweza kuwa ghali sana kwa wachezaji hao wa London. (Telegraph - usajili unahitajika)
Aston Villa wanapania kumnunua mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27. (Football Insider)
Mshambulizi wa Ureno Joao Felix hatarejea Atletico Madrid msimu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitarajiwa kuongeza mkataba wake wa mkopo Chelsea. (Sun)
AC Milan wanafuatilia hali ya winga wa Arsenal Muingereza Reiss Nelson, 23, ambaye bado hajasaini mkataba mpya na The Gunners. (Calciomercato kupitia Football Italia - kwa Kiitaliano)
AC Milan pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 27. (90min)
Manchester United wanatayarisha ofa ya kumnunua beki wa kulia wa Monaco Mbrazil Vanderson, 21, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vingine kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza. (RMC Sport kupitia Sun)
BBC