Yanga - Local

Wasimamizi uwanja wa Benjamin Mkapa wasimamishwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 May 2023
Wasimamizi uwanja wa Benjamin Mkapa wasimamishwa

Kutokana na tukio la kukatika kwa Umeme kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jana wakati wa mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rivers United, Serikali imechukua hatua ya kuwasimamisha kazi Wasimamizi wa uwanja ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo ambalo limetokea kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki sita

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana ameagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanaohusika na uendeshaji wa uwanja wa Mkapa ambao ni Kaimu Meneja wa Uwanja Salum Mtumbuka, Mhandisi wa Umeme Manyori Juma Kapesa na Afisa Tawala wa Uwanja Tusege Nikupala

Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ambao wana jukumu la kusimamia uwanja ni Gordon Nsajigwa, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano

Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa uwanja

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
59m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’