Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga SC uliopangwa kuchezwa Mei 7, 2023 katika dimba la Liti Singida mpaka utakapopangiwa tarehe nyingine.
Pia TFF imesogeza mbele siku moja mchezo wa nusu fainali nyingine kati ya Azam FC dhidi ya Simba SC ambao ulipangwa kuchezwa Mei 6, 2023 katika dimba la Nangwanda Sijaona Mtwara na badala yake mchezo huo utapigwa Mei 7, 2023
