Goli la dakika ya 85 lililofungwa na Jordi Alba liliihakikishia Barcelona ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Osasuna na kukaribia kushinda taji la La Liga msimu huu
Wakati Barcelona ikiibuka na ushindi, mahasimu wao Real Madrid wakakumbana na kipigo wasichokitarajia ugenini kutoka kwa Real Sociedad wakifungwa mabao 2-0
Ni matokeo ambayo yameifanya kazi ya Barcelona kuwa bingwa msimu huu kuwa rahisi kwani sasa wanahitaji alama mbili tu kutoka mechi tano zilizosalia
Barcelona imefikisha alama 82 kileleni mwa msimamo wakati Real Madrid ina alama 68 katika nafasi ya pili