West Ham watahitaji pauni milioni 100 kumwachia kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24, msimu huu wa joto. (ESPN)
Chelsea wanapania kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez msimu huu wa joto. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 pia analengwa na Manchester United. (Football Insider)
Chelsea wanataka kumfanya mlinda mlango wa Inter Milan na Cameroon Andre Onana, 27, nambari moja msimu ujao na wana uhakika wa kumsajili Mauricio Pochettino kama meneja wao mpya. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, atatia saini mkataba wa miaka sita na Real Madrid msimu huu, ambao utamfanya kuwa mchezaji wa pili anayelipwa pesa nyingi kwa miamba hao wa Uhispania baada ya Mshambuliaji wa Ubelgiji 32 Eden Hazard. (SER Deportivos, via Mail)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anataka kumsajili beki Mholanzi Jeremie Frimpong, 22, kutoka Bayer Leverkusen msimu huu. (Mirror)
Manchester United hawana mpango wa kumsajili Wout Weghorst kwa mkataba wa kudumu. Mshambuliaji huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na United kwa mkopo kutoka Burnley mwezi Januari. (Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, 37, anatazamiwa kuongeza mkataba wake Real Madrid hadi 2024. (Relevo - kwa Kihispania)
Manchester City wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili kipa wa timu ya taifa ya England ya chini ya miaka 16 Spike Brits kutoka AFC Wimbledon. (Fabrizio Romano)
Arsenal inawanyatia wachezaji Dinamo Zagreb mwenye umri wa miaka 23 na beki wa Croatia Josip Sutalo. (Evening Standard)
BBC



