Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya Jumapili, May 07 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2023
Tetesi za soka Ulaya Jumapili, May 07 2023

West Ham wanataka kuwasajili kiungo wa kati wa Manchester City na England Kalvin Phillips, 27, na beki wa kulia Kyle Walker, 32. (90min).

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, amehusishwa na kuhamia klabu ya Saudi Arabia Al Hilal - uhamisho ambao utamfanya mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 33, kuondoka katika klabu hiyo. (Sky Sports)

PSG wanataka Messi abaki na wamempa ofa bora zaidi ya kifedha kutoka klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Sunday Times)

Kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 25, anatazamiwa kusaini mkataba mpya huko Newcastle ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo. (Football Insider)

Juventus wanataka kumsajili mshambuliaji wa England Mason Greenwood, 21, kwa mkopo kutoka Manchester United. (Sun Sunday)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Mason Mount, 24, anasakwa sana na Liverpool. (Mail Sunday)

Kiungo wa kati wa Brighton mwenye umri wa miaka 24 Alexis Mac Allister, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina, "anatamani sana" kujiunga na Liverpool. (Football Insider)

Winga wa Brazil Raphinha, 26, anafikiria kuondoka Barcelona msimu huu wa joto. Arsenal wanamtaka mchezaji huyo wa zamani wa Leeds, huku Chelsea na Newcastle pia zikimtaka. (Sport)

Tottenham huenda ikalazimika kuilipa Bayern Munich pauni milioni 10 kama fidia ili kumpata Julian Nagelsmann kuwa kocha wao mkuu mpya. (Sunday Telegraph)

Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ndiye chaguo kuu la mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer, 29, bado hajafanya mazungumzo kuhusu mustakabali wake na mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel. Sabitzer kwa sasa yuko kwa mkopo Manchester United. (Sky Germany, via Manchester Evening News)

Manchester City na Arsenal zote zinataka kumsajili kiungo wa kati wa AC Milan na Algeria Ismael Bennacer, 25. (FootballTransfers)

Kiungo wa kati wa zamani wa Hispania na Barcelona Andres Iniesta, 38, anatarajiwa kuondoka Vissel Kobe ya Japan msimu wa joto. (Nikkan Sports)

Kiungo wa kati wa Bournemouth na Colombia Jefferson Lerma, 28, anasakwa na West Ham, Crystal Palace na Leicester. (TeamTalk).

Bosi wa zamani wa Barnsley na West Brom Valerien Ismael anaiwania nafasi ya Chris Wilder kuwa kocha mkuu wa Watford. (Athletic)

Manchester City wanataka kuanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa kiungo wa kati James McAtee, 20, baada ya kuwa na mchango mkubwa katika kuipandisha daraja Sheffield United alipokuwa kwa mkopo Bramall Lane. (Mail on Sunday)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’