Simba imeondoshwa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam Fc
Mwaikenda na Prince Dube walifunga mabao ya Azam Fc wakati Sadio Kanoute akifunga bao pekee la Simba
Ulikuwa mchezo uliotawaliwa na matumizi ya nguvu huku Azam Fc wakiwa bora katika safu yao ya ulinzi wakihakikisha wanadhibiti safu ya ushambuliaji ya Simba iliyoongozwa na Jean Baleke, Chama na Saido Ntibazonkiza
Azam Fc inatinga fainali na kusubiri mshindi wa mchezo kati ya Singida BS dhidi ya Yanga utakaopigwa May 21
Kwa Simba ni msimu ambao wanakwenda kuhitimisha bila kushinda taji lolote!


