Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba - Azam - Local

Rais Samia apewa heshima Ligi Kuu Marekani

Joel JJ By Joel JJ
8 May 2023
Rais Samia apewa heshima Ligi Kuu Marekani

Mashabiki wa soka takribani 31,620 waliohudhuria mechi ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na mamilioni zaidi duniani waliokuwa wakitazama mbashara mechi ya Seattle Sounders dhidi ya Sporting Kansas City kupitia FOX TV na Apple TV, wamepata fursa ya kushuhudia Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania akienziwa katika tukio maalum kabla ya mechi hiyo kuanza mjini humo jana Jumapili Mei 7, 2023

Mmiliki wa Seattle Sounders, Bilionea Adrian Hanauer, aliamua kutumia mechi hiyo kufanya tukio la kumpongeza Rais Samia kwa hatua zake za kutangaza utalii wa Tanzania hasa kupitia filamu ya Royal Tour

Kwa heshima hiyo, Hanauer jana alitumia mechi hiyo kukabidhi jezi maalum yenye jina la Rais Samia kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi na ujumbe wake na zaidi kutoa heshima kwa ujumbe wa Tanzania kupiga picha maalum na kikosi cha Sounders kabla ya kuanza kwa mechi hiyo muhimu

"Lengo la tukio hili maalum kwa Rais wa Tanzania ni kutambua mchango wake katika kutangaza utalii," alisema Hanauer na kuongeza:

"Niliwahi kutoa mchango mwingine kwa kuileta timu hii mwaka 2005 Tanzania ikacheza na klabu kubwa za Simba na Yanga na tutaangalia tena jinsi ya kufanya ziara nyingine ya kiutalii kuja Tanzania na wachezaji wetu," alisema

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi amesema kuwa tukio hilo ni heshima kubwa kwa Rais Samia, nchi ya Tanzania na utalii wa Tanzania

"Mamilioni ya watu waliofuatilia leo matukio ya uwanjani watazidi kujihusisha na brand ya Tanzania na kuja nchini," alisema Dk Abbasi akiwa uwanjani hapo

Tukio la jana linakuja ikiwa ni siku chache tu baada ya juzi ambapo wamiliki wa Seattle Sounders walitoa fursa nyingine ya kuutangaza utalii wa Tanzania katika sehemu ya uwanja huo kwa kuionesha filamu ya Tanzania; "The Royal Tour" kwa wawakilishi wa kampuni kubwa duniani kama Google, Boeing, Starbucks, Amazon, Delta, Microsoft na ofisi ya Meya wa Seat

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
6h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
7h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
9h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
9h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
10h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
10h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
11h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
11h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
11h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
13h ago
READ MORE →