Manchester United wako tayari kusukuma nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Muingereza Declan Rice, 24, lakini Arsenal bado wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili. (Guardian)
Kiungo wa kati wa Marseille na Ufaransa Matteo Guendouzi, 24, anaweza kuchukua nafasi ya Rice katika klabu ya West Ham.(Mirror)
Chelsea na Manchester United wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 30, huku Tottenham pia wakiwa mawindoni kusaka mlinda mlango mpya. (Mirror)
Chelsea itamruhusu mlinzi wa Brazil Thiago Silva, 38, kujiunga tena na Fluminense msimu huu wa joto. (Telegraph)
Manchester United wameanza mazungumzo na beki wa Napoli wa Korea Kusini Kim Min-jae. Liverpool na Paris St-Germain pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (FootMercato)
Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza, Jude Bellingham, 19, amekubaliana masharti binafsi na Real Madrid.(90min)
Tottenham wanatarajiwa kukamilisha usajili wa kudumu wa mshambuliaji wa Sweden Dejan Kulusevski, 23, kutoka Juventus msimu huu wa joto. (PA via Independent) Tottenham wako tayari kumfanya mlinzi wa Roma Mbrazil Roger Ibanez, 24, kuwa usajili wao wa kwanza katika dirisha la msimu wa joto. (La Repubblica via Four Four Two)
Brighton wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Mahmoud Dahoud, 27, wakati kandarasi yake ya Borussia Dortmund itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Jesse Lingard, 30, amepata ofa ya kujiunga Besiktas mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu. (Nottingham Post)
Arsenal wanavutiwa na mlinzi wa RB Leipzig mwenye umri wa miaka 23 Mfaransa Mohamed Simakan, ambaye alisaini mkataba mpya mwezi Disemba. (Guardian)
Tottenham na Manchester United lazima walipe pauni milioni 40 ikiwa wanataka kumsajili kipa wa Hispania David Raya, 27, kutoka Brentford msimu huu wa joto. (Evening Standard)
Newcastle inaweza kutoa pauni milioni 30 kumnunua mchezaji wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 23, Amine Adli, ingawa wanatarajia ushindani kutoka kwa Bayern Munich na AC Milan
BBC