Hersi autaka ubingwa Shirikisho Afrika

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th May 2023


Hersi autaka ubingwa Shirikisho Afrika

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wamekwenda Afrika Kusini wakiwa na malengo ya kupata matokeo mazuri ambayo yatawavusha hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Hersi ameongoza msafara wa Yanga uliotua Afrika Kusini jana kuelekea mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya Shirikisho dhidi ya Marumo Gallanst ambao utapigwa Jumatano May 17 Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-0

Hersi amesema kwa hatua waliyofika katika michuano ya CAF CC, wanayo nafasi ya kutinga fainali na pengine kutwaa ubingwa

Hersi ambaye juzi aliongoza shamrashamra za kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Azam Complex, amesema itakuwa heshima kubwa kwa klabu ya Yanga kuwa timu ya kwanza kufika fainali ya kombe la Shirikisho na hata kuwa bingwa

"Nawapongeza Wanayanga lakini nataka nikuhakikishie sisi kwa pamoja kazi hii hatujaimaliza, kazi itamalizika Jumatano kuipeleka Tanzania kwenye fainali ya Mashindano haya na Mungu akijaalia tutakuwa Klabu ya kwanza kuleta Kombe la Afrika"

"Niweke sawa kulikuwa na kombe linaitwa CAF Cup kombe hilo ndio wenzetu walifika Fainali, kulikuwa na shindano lingine linaitwa CAF Winners Cup (Kombe la Washindi) mashindano haya yaliunganishwa mwaka 2004 yakatengeneza CAF Confederation Cup hili ni kombe kubwa liliounganisha mashindano mawili ( CAF Cup & CAF Winners Cup )"

"Yanga ndio Klabu ya kwanza kutoka Tanzania kushiriki mashindano haya kwenye ngazi ya Nusu Fainali , lakini Yanga iko mguu mmoja kuelekea Fainali , hajawahi kushiriki yoyote kutoka Tanzania kombe hili hatua ya Nusu fainali," alisema Hersi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.