Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne, May 16 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne, May 16 2023

Nyota wa Manchester City Bernardo Silva anasakwa zaidi na Paris St-Germain wanaotaka kumleta kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 28 kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35. (Le Parisien)

Arsenal wako tayari kuipa West Ham kiasi cha £90m ambayo ni rekodi ya klabu kwa ajili ya kiungo wa kati wa England Declan Rice, 24, wakati Granit Xhaka wa Switzerland, 30, anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaouzwa na The Gunners. (Mail)

Kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Manchester United, anataka kujiunga na klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ataondoka Brighton msimu huu wa joto. (Athletic)

Meneja mpya mtarajiwa wa Chelsea Mauricio Pochettino anatazamiwa kufanya mazungumzo na Mason Mount ili kumshawishi kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 24 kuongeza mkataba wake ambao unamalizika msimu wa joto wa 2024. (Football Insider)

Bayern Munich na Borussia Dortmund zote zinamtaka kiungo wa kati wa Mexico Edson Alvarez, 25, ambaye Ajax inaweza kuwa tayari kumuuza kwa £30m. (SPORT1)

Mabeki wa Uingereza Phil Jones, 31, na Axel Tuanzebe, 25, wanatarajiwa kuuzwa na Manchester United msimu huu wa joto. (ManchesterEveningNews)

Newcastle pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Conor Gallagher, wakati The Magpies watakabiliana na ushindani kutoka kwa Tottenham wanaomtaka mchezaji mwenzake wa kimataifa wa England anayekipiga Leicester City James Maddison. (Mail)

Manchester United wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Borussia Dortmund Gregor Kobel, ingawa klabu hiyo ya Ujerumani inakusudia kumpa mkataba mpya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 25. (Independent)

Tottenham wamefanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa Roma kuhusu jukumu lao la mkurugenzi wa soka. (The i Newspaper)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
21h ago
READ MORE β†’