Katibu Mkuu wa Klab ya Pamba Johnson James amesema, wameandaa Mawakili wa wanne ambao wataiandikia barua kamati ya maadili ya FIFA wakitaka klabu ya Kitayosce Fc ishushwe daraja
Ni baada ya timu hiyo kukutwa na hatia ya upangaji wa matokeo katika mchezo Championship dhidi ya Fountain Gate
Pamba Fc ilimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Championship nyumba ya Kitayosce iliyomaliza nafasi ya pili na kupanda ligi kuu
Pamba itacheza play-off kusaka nafasi ya kupanda ligi kuu lakini uongozi wa timu hiyo unaamini Kitayosce ilipaswa kushushwa daraja baada ya kukumbwa na kashfa ya kupanga matokeo
Kama Kitayosce itashushwa daraja basi Pamba watapanda moja kwa moja ligi kuu
ADVERTISE HERE