Pamba - Local

RC Malima aipa sapoti Pamba Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 May 2023
RC Malima aipa sapoti Pamba Fc

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima anaamini timu ya Pamba inayoshiriki ligi ya 'Championship' bado ina nafasi ya kupanda ligi kuu

Malima amesema hayo leo alipozunguza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo. Malima amesema kuwa timu hiyo imeonyesha uwezo mkubwa katika michezo yao hivyo ina uwezo wa kucheza ligi kuu kikubwa wachezaji waongezee bidii

"Sina shaka na nyie uwezo wenu nimeuona uwanjani naamini benchi la ufundi litafanyia marekebisho eneo la umaliziaji ili muweze kufunga magoli mengi," amesema Malima

Katika hatua nyingine Malima amewasii viongozi pamoja na timu kwa ujumla kufanya maandalizi mazuri ili waweze kushinda mchezo ujao wa mchujo dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma Mei 21 mwaka huu ili kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Mei 28 kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza

Amewakabidhi wachezaji wa Pamba kiasi cha Sh milioni 3 ambapo ahadi yake ilikuwa Sh milioni 1na Sh milioni mbili kutoka kwa Jambo food products.

Timu ya Pamba FC imemaliza michezo ya ligi hiyo kwa msimu huu ikiwa nafasi ya tatu mbele ya Kitayose fc ya na Jkt Tanzania ambazo zimepata nafasi ya kupanda ligi kuu moja kwa moja hivyo timu ya Pamba itacheza mchezo wa mchujo dhidi ya Mashuja fc ya Kigoma iliyomaliza nafasi ya nne

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’