Tottenham wanaweza kuchukua hatua ya kushangaza kwa kumnunua mlinda lango wa Chelsea kutoka Senegal Edouard Mendy, 31, huku wakitafuta mbadala wa mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris, 36, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
Mlinzi wa Manchester United na England Harry Maguire anaweza kuhamia West Ham au Tottenham huku mchezaji huyo wa miaka 30 akiwa hapendwi tena na mkufunzi Erik ten Hag. (Football Transfers)
Meneja wa muda wa Chelsea Frank Lampard anasema alijaribu kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Haaland katika kipindi chake cha kwanza Stamford Bridge, kabla ya mchezaji huyo wa miaka 22 kuhamia Borussia Dortmund. (Mail)
William Saliba anavutia vilabu vitatu ambavyo havikutajwa, huku Arsenal wakiendelea kujadiliana kuhusu mkataba mpya na beki huyo wa kati wa Ufaransa, 22. (Mirror)
Tottenham ndio washindani wakuu kwenye uwaniaji wanafasi ya mkufunzi wa Feyenoord Arne Slot kama meneja wao mpya mwishoni mwa msimu huu, huku timu hiyo zi ikihofia kutaka kuhamia Uingereza. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, anaripotiwa kutaka kuhamia AC Milan, ambao wamemchagua kama kipaumbele cha kwanza wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Fabrizio Romano)
Mmiliki mwenza wa Crystal Palace Steve Parish amemmwagia sifa meneja Roy Hodgson kabla ya mazungumzo ya kandarasi kati ya kocha huyo mkongwe na klabu hiyo. (Standard)
Kipa wa Palace na England Jack Butland, 30, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Manchester United, anakaribia kukubali kuhamia Rangers msimu huu wa joto. (Mail)
Kufuatia tangazo la kuondoka kwake Manchester United, mlinzi wa Uingereza Phil Jones, 31, "anachukua muda" kutafakari hatua yake inayofuata. (Lancashire Telegraph)
Wakala wa mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 30, hivi majuzi alikutana na Fenerbahce ya Uturuki, na kuchochea tetesi kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anaweza kuondoka msimu huu. (Goal)
Lucas Moura anatathmini chaguo lake baada ya kuamua kuondoka Tottenham, huku vilabu vya Saudi Arabia, Ligi Kuu ya Soka na Serie A vikiwa vimewasiliana na mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30. (Fabrizio Romano)
West Ham itamruhusu meneja David Moyes kujiamulia mustakabali wake ikiwa atawaongoza kutwaa ubingwa wa Europa Conference League. (Mail)
Beki wa kati wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26, amefanya mazungumzo ya awali na Paris St-Germain, huku miamba hao wa Ufaransa wakiungana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumnasa beki wa Napoli. (Mirror)
PSG wanatazamia kuongeza juhudi zao za kumnasa Jose Mourinho kutoka Roma, huku wachezaji wa karibu na meneja huyo wa Ureno wakihofia kuwa ataondoka katika klabu hiyo ya Italia msimu huu wa joto. (Mail)
Manchester United na Chelsea zitamenyana moja kwa moja kupata huduma za mshambuliaji wa Gent wa Nigeria Gift Orban, 20. (FourFourTwo)
BBC