Simba - Local

Tutafanya usajili bora - Ahmed

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 May 2023
Tutafanya usajili bora - Ahmed

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema baada ya msimu huu kukamilika, mchakato wa maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao utaanza mara moja

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Bodi ya Ligi, mechi za kuhitimisha msimu zitapigwa Juni 09 ambapo katika mwezi huo dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa

Ahmed amesema uongozi wa Simba unafahamu kiu ya mashabiki ni kuona timu yao inaboreshwa zaidi ili kuhakikisha kilichotokea msimu huu hakijirudii msimu ujao

Aidha Simba itashiriki mashindano mapya ya Super League yatakayohusisha timu nane vigogo barani Afrika, hivyo kuwa na ulazima wa kufanya maboresho haraka ili benchi la ufundi lipate muda wa kutosha kukiandaa kikosi

"Uongozi unafahamu kiu ya mashabiki wa Simba ni usajili hasa kutokana na kile kilichotokea msimu huu ambao hatujaweza kushinda taji lolote"

"Uongozi unafanya kazi kwa karibu na benchi la ufundi ili kuhakikisha usajili utakaofanyika utazingatia mahitaji ya timu. Tunawaambia Wanasimba, tumejipanga safari hii tutaleta watu kwelikweli," alisema Ahmed

Tayari Simba imeanza kuhusishwa na baadhi ya wachezaji pamoja na kuwa kwa wakati huu bado ni tetesi tu

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
28m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’