Bayern Munich wanamwona Declan Rice kama kiungo bora zaidi wa safu yao ya ulinzi lakini wanafahamu fika kuwa Arsenal pia wanapania kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 24. (Sky Sport Germany)
Manchester United wako kwenye mazungumzo juu ya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Brazil Neymar, 31, kutoka Paris St-Germain. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Man United pia wanajaribu kukamilisha dili la kumnunua mchezaji wa Napoli Kim Min-jae, 26, huku PSG wakimtaka beki huyo wa Korea Kusini pia. (Sua)
Barcelona wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 26, kutoka Wolves msimu huu wa joto lakini hatua hiyo inategemea ikiwa mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati, 20, ataondoka kwanza Barca. (The Athletic- Usajili unahitajika)
Ikiwa Arsenal hawatafanikiwa kumsajili Rice, wamewapanga Neves, kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 24, na kiungo wa kati wa Brighton wa Ecuador Moises Caicedo, 21, kama mbadala. (Mail)
Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 30, anasema mustakabali wake utaamuliwa kabla ya mechi ya mwisho ya Arsenal msimu huu, huku The Gunners wakipiga hatua katika mazungumzo yao na Bayer Leverkusen kuhusu uhamisho wa pauni milioni 13. (Standard)
AC Milan wamemfanya Folarin Balogun wa Arsenal kuwa mlengwa wao mkuu wa uhamisho baada ya mshambuliaji huyo wa Marekani, 21, kuonyesha kiwango cha juu cha mchezo wake wakati alipokuwa Reims kwa mkopo msimu huu, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa RB Leipzig. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Vinicius Junior hana mpango wa kuondoka Real Madrid, licha ya winga huyo wa Brazil, 22, kukumbwa na dhuluma za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki wa wapinzani. (90 Min)
Liverpool wamejiunga na orodha ndefu ya vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Uingereza Marc Guehi, 22, kutoka Crystal Palace. (Mail)
Liverpool wanakaribia kuafikiana na kiungo wa kati wa Brighton mwenye umri wa miaka 24 na Argentina Alexis Mac Allister. (Fabrizio Romano)
Manchester United wako tayari kumwacha Anthony Martial aondoke baada ya kushindwa kumvumilia mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 27. (Sun)
BBC