Azam - Yanga - Local

Azam Fc yapania alama sita za kuhitimisha msimu

Joel JJ By Joel JJ
24 May 2023
Azam Fc yapania alama sita za kuhitimisha msimu

Azam Fc kwa sasa hawaifikirii fainali ya kombe la Shirikisho (FA) badala yake akili zao zipo kwenye michezo yao miwili ya mwisho ya ligi kuu Tanzania Bara ambapo wanataka kumaliza vizuri mechi hizo za mwisho msimu huu

Azam FC imetinga Fainali ya FA ikitarajia kucheza na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, na kwenye ligi inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 53 ikipishana kwa pointi mbili dhidi ya Singida Big Stars yenye pointi 51 wakivutana kumaliza katika nafasi hiyo.

Afisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria amesema kuwa wanachokiangalia hivi sasa ni mechi zao mbili za ligi kuhakikisha wanaibuka na pointi sita zilizobakia kwa kuwa fainali ya FA bado haijapangwa.

"Hii mechi ya FA bado hatujui itachezwa lini kwa sababu TFF bado hawajaipangia ratiba, hatuwezi kuifikiria kwa sasa, sisi tunaelekeza nguvu kwenye michezo yetu miwili ya mwisho kwenye ligi na baada ya hapo ndipo tutaanza mikakati kwa mchezo huo wa fainali baada ya kufahamu tarehe ya mchezo," alisema Zaka

Alisema kujiandaa na michezo hiyo miwili ya mwisho, awali waliweka kambi lakini baada ya bodi ya ligi kupangua ratiba waliamua kuvunja kambi na kuwapa wachezaji wao mapumziko mafupi.

"Lakini kwa sasa wachezaji wamerejea kwenye mazoezi kujiandaa na michezo hii miwili, malengo yetu ni kuhakikisha tunamaliza vizuri ligi msimu huu kwa kusanya pointi zote sita zilizosalia," alisema Zaka.

Bodi ya ligi imetangaza michezo ya mwisho kuhitimisha msimu huu wa ligi kuu itachezwa Juni 9.

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
56m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →