Klabu ya Simba imemteua Mels Daalder kuwa skauti wa Mkuu wa Klabu hiyo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Simba, Mels ni raia wa Uholanzi mwenye uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali
Mels ameshiriki kozi mbalimbali za scouting duniani ikiwa ni pamoja na kozi zikizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson
Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania, ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na ana ujuzi mkubwa na ufahamu mkubwa wa ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika
Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo; Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani. Pia kwa Vipindi Tofauti amewahi fanya kazi baadhi ya Wachezaji na vilabu ikiwapo Mtibwa sugar na Coastal Union