Takwimu zaibeba Yanga mechi dhidi ya USM Agler

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th May 2023


Takwimu zaibeba Yanga mechi dhidi ya USM Agler

Kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga dhidi ya USM Algers hizi ni namba muhimu kuelekea mchezo huo mkubwa Afrika

Kuanzia hatua ya makundi timu hizo zimecheza michezo kumi hadi sasa. Yanga wameshinda michezo saba wamepoteza mchezo mmoja, na kutoa sare michezo miwili, huku USM Algers wakishinda michezo mitano, sare michezo mitatu na kupoteza michezo miwili

Yanga wamefunga jumla ya magoli 15 hadi sasa kwenye michuano hiyo, mabao tisa wamefunga katika uwanja wa nyumbani, huku mabao sita wakifunga viwanja vya ugenini

Yanga wameruhusu jumla ya mabao matano, mabao manne wameruhusu katika viwanja vya ugenini, huku wakiruhusu kufungwa bao moja kwenye uwanja wa nyumbani

USM Algers wamefunga jumla ya mabao 17, mabao 13 wamefunga katika uwanja wa nyumbani huku mabao manne wakifunga kwenye viwanja vya ugenini

USM Algers wameruhusu nyavu zao kuguswa mara nane, mabao saba wamefungwa katika viwanja vya ugenini huku wakiruhusu bao moja tu kwenye uwanja wa nyumbani

Jumapili ni fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho Afrika baina ya timu hizo mbili zenye namba za kusisimua kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu Afrika ,ambapo mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa DSM na kisha mchezo wa mkondo wa pili kupigwa nchini Algeria Juni 3, mwaka huu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.