Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa May 26 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa May 26 2023

Mshambulizi wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, anasema alijua kuwa klabu hiyo ya Italia ingejaribu kumsajili ikiwa uhamisho wake kwenda Chelsea hautafanikiwa. (Mail)

Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane, 29, kiungo wa kati wa West Ham, 24, Declan Rice na kiungo wa kati wa Chelsea Mason Mount, 24, msimu huu wa joto, huku mchezaji huyo akiwa kipaumbele kikuu cha wachezaji hao watatu wa kimataifa wa Uingereza. (Sky Sports)

United wameanza mazungumzo na mama na wakala wa kiungo wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, kwa nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa uhamisho wa bure. (Nicolo Schira)

Tottenham wanamfikiria sana mkufunzi wa Celtic, Muaustralia, Ange Postecoglou kama mgombea wa nafasi yake ya umeneja baada ya Arne Slot kuamua kusalia Feyenoord. (Independent)

Spurs pia wamewasiliana na meneja wa zamani wa Leicester Brendan Rodgers, huku mkufunzi wa zamani wa Chelsea Graham Potter na kocha mkuu wa zamani wa Uhispania Luis Enrique pia wakiwa kwenye orodha ya walioteuliwa na klabu hiyo. (Football Transfers)

Hata hivyo, Enrique pia ameibuka kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa Paris St-Germain Christophe Galtier. (Goal)

Chelsea na Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, lakini klabu yake ya zamani ya Manchester City haiko mbioni kumsajili kiungo huyo wa kati wa Southampton. (Times - usajili unahitajika)

AC Milan imemfanya kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, kuwa lengo kuu msimu huu. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 26, pamoja na mlinzi wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 25, wananyatiwa na Newcastle United msimu huu wa joto huku wakipania kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (i Sport)

Qatar Sports Investments, ambao wanamiliki Paris St-Germain, wamefanya harakati za kuwanunua mabingwa mara nane wa Serie A wa Brazil, Santos. (Mirror)

Aston Villa wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Leicester City mwenye umri wa miaka 25, Harvey Barnes. (Independent)

West Ham pia wanavutiwa na Barnes, pamoja na winga wa Leeds United Muingereza Jack Harrison, 26. (Sun)

Fulham wanajadiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Brazil Willian ili kuongeza muda wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kusalia Craven Cottage kwa msimu mwingine. (Fabrizio Romano)

Everton wamewasiliana na kocha mkuu wa Botafogo Luis Castro, 61, wakati wanajadili kuchukua nafasi ya Sean Dyche kama meneja msimu huu. (Daily Record)

Paris St-Germain wamewasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Uruguay Manuel Ugarte, huku Chelsea pia wakiwa katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano)

Mshambulizi wa Argentina Angel di Maria anatazamiwa kuondoka Juventus kama mchezaji huru msimu huu wa joto, huku klabu kadhaa za MLS na Saudi Arabia zikitaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35. (90 Min)

Beki wa Ureno Diogo Dalot, 24, yuko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Manchester United. (Fabrizio Romano)

Newcastle na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa kati wa Swansea City na Scotland Azeem Abdulai, 20. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’