Yanga yatua Algeria

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st June 2023


Yanga yatua Algeria

Msafara wa Yanga umewasili salama Algeria tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, Juni 03 katika uwanja wa July 05 1962, saa 4 usiku

Msafara wa takribani watu 253 utakuwa Algeria kwa siku tatu, ukijumuisha wachezaji 29, benchi la ufundi, viongozi waandamizi wa Yanga na Serikali kupitia Wizara ya Michezo, TFF na mashabiki

Yanga itakuwa na siku moja ya kukamilisha maandalizi yake kabla ya mtanange wa fainali siku ya Jumamosi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.