Yanga yafa kiume Algeria

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th June 2023


Yanga yafa kiume Algeria

Ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya USM Alger haukutosha kuipa Yanga nafasi ya kutwaa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya USM Alger kushinda taji kwa faida ya mabao ya ugenini

Dakika 180 za mchezo zimemalizika kwa sare ya mabao 2-2 lakini ushindi wa mabao 2-1 ambao USM Alger walipata uwanja wa Benjamin Mkapa umewanufaisha kutwaa taji la Shirikisho

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Djuma Shaban kupitia mkwaju wa penati baada ya Kennedy Musonda kufanyiwa madhambi kwenye dakika ya tano

Ulikuwa mchezo uliotawaliwa na vurugu nyingi kutoka kwa mashabiki ambapo mechi ilisimamishwa mara mbili kutokana na moshi kutanda uwanjani

USM Alger inakuwa timu ya kwanza kushinda kombe la Shirikisho katika nchi ya Algeria


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.