Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania yamekamilika
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mgunda alisema Simba inauchukulia mchezo huo kwa uzito sawa na michezo mingine waliyocheza kabla
"Mchezo wa kesho ni muhimu kama ilivyo mechi nyingine, ingawa matokeo hayatabadili chochote kwetu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda"
"Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa kesho isipokuwa Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda," alisema Mgunda
Mchezo huo utapigwa kesho Jumanne, saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex
Ni moja ya mechi mbili za kuhitimisha msimu mchezo wa mwisho ni dhidi ya Coastal Union siku ya Ijumaa