Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Juni 06 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Juni 06 2023

Mchezaji wa Manchester City Ilkay Gundogan, 32, huenda akarejea Borussia Dortmund msimu huu wa joto kwa sababu Barcelona hawana uwezo wa kulipa mshahara wa kiungo wa kati wa Ujerumani ambaye mkataba umemalizika. (Bild - kwa Kijerumani)

Barca wamejaribu kumshawishi Gundogan kwa kuongeza ofa yao ya mkataba hadi miaka mitatu na kupunguzwa mishahara, wakati Arsenal wametoa mkataba wa miaka miwili na pendekezo la faida kubwa pia linatarajiwa kutoka kwa klabu ya Saudi. (Sport - kwa Kihispania)

Dau la kwanza la Real Madrid kwa Harry Kane litakuwa la euro milioni 80 (£69m) lakini Tottenham awali wamemthamini mshambuliaji huyo wa Uingereza, 29, kwa euro milioni 120. (£103m). (Sport - Kwa Kihispania)

Tottenham itamsaidia meneja anayekuja Ange Postecoglou na fedha za kuchuana na Newcastle kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Leicester na Uingereza James Maddison, 26, na kulenga kipa wa Brentford Uhispania David Raya, 27, na beki wa Wolves Muingereza Max Kilman, 26. (Mirror)

Paris St-Germain wameshinda Chelsea katika mbio za kumsajili kiungo wa Uruguay Manuel Ugarte, 22, kutoka Sporting Lisbon. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Chelsea wameelekeza nguvu zao kwa usajili wa kiungo wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, baada ya kumkosa Ugarte. (Standard)

Chelsea pia wamefufua nia yao ya kumnunua kiungo wa Southampton na Ubelgiji Romeo Lavia, 19 - na mshambuliaji wa zamani wa The Blues Eden Hazard amekuwa na jukumu katika uhamisho unaotarajiwa. (Express)

Alexis Mac Allister atajiunga na Liverpool kutoka Brighton, akifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, huku kiungo huyo wa kati wa Argentina, 24, akisadikiwa kuwa amekubali kandarasi ya miaka mitano. (Standard)

Atletico Madrid wameuliza kuhusu uwezekano wa kumnunua Wilfried Zaha. Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast, 30, atakuwa mchezaji huru iwapo ataamua kutokubali mkataba mpya na Crystal Palace. (Mail)

Liverpool wako tayari kulipa Barcelona euro milioni 35 (£30m) kumsajili kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 26. (Sport - in Spanish)

Tottenham wamewasiliana na Everton kuhusu uwezekano wa kumnunua mlinda mlango wa England Jordan Pickford msimu wa joto lakini huenda ikarudishwa nyuma na bei ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye yuko chini ya mkataba hadi 2027. (Football transfer)

Aston Villa wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji huru Youri Tielemans, 26, baada ya kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji kuondoka Leicester. (The Athletics)

Kipa wa Ureno Diogo Costa, 23, amepuuza tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kutoka Porto hadi Manchester United msimu huu wa joto. (Mail)

N'Golo Kante bado yuko tayari kusalia Chelsea lakini kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 32, bado hajakubali mkataba mpya na vilabu vya Saudi Al Ittihad na Al Nassr vina nia ya kumsajili msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Newcastle United wamefahamishwa kwamba kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, ananuia kusalia Manchester City. (Telegraph - usajili unahitajika)

Newcastle wameongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Uturuki Arda Guler, 18, kutoka Fenerbahce. (Football Insider)

Real Madrid wameiuliza Bayern Munich kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Canada Alphonso Davies, 22. (Marca - kw Kihispania)

Inter Milan wamefanya mpango wa kumsajili beki Mwingereza Trevoh Chalobah, 23, kutoka Chelsea msimu huu. (Football Insider)

Brighton wanatarajiwa kutangaza kuwasili kwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mahmoud Dahoud, 27, kutoka Borussia Dortmund kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)

West Ham inawafuatilia viungo watatu - Muingereza James Ward-Prowse, 28, wa Southampton, Muingereza Conor Gallagher, 23, wa Chelsea na Scott McTominay wa Scotland, 26 wa Manchester United. (Football Transfers)

Beki wa Sweden Victor Lindelof, 28, anatazamiwa kuongezewa mkataba mpya na Manchester United. (Sun)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
32m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
44m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’