Kiungo mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza usiku wa kuamkia leo aliibuka na tuzo tatu katika hafla ya utolewaji tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2022/23
Saido alishinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu, kiungo bora wa Ligi Kuu na tuzo ya FAIR PLAY

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ndiye mchezaji bora wa msimu akiondoka na tuzo tatu, mfungaji bora na tuzo kubwa ya MVP pamoja na tuzo ya goli bora la msimu
Mayele yuko Cameroon katika majukumu ya timu ya Taifa, tuzo zake zilipokewa na mkewe kwa niaba yake
Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi akaondoka na tuzo ya kocha bora wa msimu wakati Dickson Job akiondoka na tuzo ya beki bora wa msimu
Clement Mzize nae akabeba tuzo ya mchezaji bora chipukizi wakati Djigui Diarra akiondoka na tuzo ya kipa bora kombe la FA na Ligi Kuu
Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto akabeba tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Simba imetoa wachezaji sita katika kikosi cha msimu huku Yanga ikitoa wachezaji wanne na mmoja kutoka Singida BS
Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Hennock Inonga, Mzamiru Yassin, Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza wa Simba wamejumuishwa katika kikosi hicho wakati Djigui Diarra, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto na Fiston Mayele ni upande wa Yanga wakati Bruno Gomez akitokea Singida BS