Swali kubwa ambalo mpaka sasa halina majibu huko barani Ulaya ni kwamba wapi ataelekea mshambuliaji Kylian Mbappe kutoka Paris Saint Germain, badaa ya taarifa kuwa klabu hiyo inapanga kumuuza Mfaransa huyo msimu huu wa joto
Imeripotiwa kuwa hatua hiyo ni baada ya PSG kuhofia huenda ikampoteza bure mchezaji huyo kwakuwa mkataba wake umebaki mwaka mmoja huku akigoma kuongeza mkataba mwingine
Awali kulikuwa na taarifa ya tarehe ya mwisho ya Julai 31, 2023 kwa Mbappe, 24, kuwaambia PSG kama angebaki PSG hadi 2025
Baada ya mazungumzo miezi kadhaa, Mbappe alitoa barua kuwa hatofanya hivyo
Hata hivyo, wakati mabingwa hao wa Ufaransa wakijaribu kurekebisha sera yao ya ujenzi wa timu baada ya miaka mingi ya kununua wachezaji nyota bila mkakati madhubuti, PSG wameazimia kutomwachia Mbappe bure, huku klabu hiyo ikikerwa na barua hiyo kuvujishwa kwenye vyombo vya habari kabla
Real Madrid wanamtamani kwa muda mrefu Mfaransa huyo na alikataa kuhamia Bernabeu kusalia PSG mwaka jana
Kuondolewa kwa Karim Benzema kwenda Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real inahitaji mshambuliaji, ingawa ilifikiriwa kuwa Harry Kane wa Tottenham alikuwa kileleni mwa orodha yao
Mbappe, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017 kwa mkopo akitokea Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m, amefunga mabao 212 katika michezo 260
Ana mabao 38 katika mechi 68 alizoichezea Ufaransa, ikiwa ni pamoja na hat-trick katika fainali ya kombe la Dunia mwaka jana nchini Qatar, Ufaransa iliposhindwa na Argentina kwa mikwaju ya penalti
Mbappe alimaliza kama mfungaji bora wa Ligue 1 katika kila misimu mitano iliyopita na ameshinda mataji matano ya ligi katika misimu yake sita akiwa PSG.