Klabu ya Yanga imeanza mchakata wa kusaka kocha mpya ambaye atarithi mikoba ya Nasreddine Nabi aliyetimkia Kaizer Chiefs
Zilianza kama tetesi lakini ni rasmi Yanga imethibitisha kuwa Nabi ameondoka baada ya kuutaarifu uongozi kuwa hataongeza mkataba
Aidha Yanga huenda ikalazimika kusuka upya benchi lake la ufundi kwani taarifa kutoka Afrika Kusini zimebainisha kuwa kocha huyo ameitarifu Kaizer Chiefs kuwa anakwenda na wasaidizi wake
Klabu ya Yanga imemtakia Nabi kila la kheri, Wananchi wataendelea kukumbuka mafanikio makubwa aliyoipatia Yanga katika misimu yake miwili