Manchester United wamemaliza nia yao ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, kutoka Tottenham msimu huu wa joto kwa kuwa wanahisi ada hiyo itakuwa juu sana. (Gardian)
Newcastle wanakaribia kukubali mkataba wa pauni milioni 50 na Inter Milan kwa kiungo wa kati wa Italia Nicolo Barella, 26. (Telegraph – Subscription required)
Arsenal wanawania sana kumsajili Kai Havertz kutoka kwa wapinzani wao wa London Chelsea, ambao watahitaji pauni milioni 70 kwa fowadi huyo wa Ujerumani, 24. (Guardian)
Juventus wanataka angalau euro 80m (£68m) kwa Dusan Vlahovic, lakini Chelsea wamewaambia Waitaliano kwamba wanaweza kuchagua kati ya wachezaji watano katika makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji huyo wa Serbia, 23. (Gazzetta dello Sport, via Football Italia)
Wachezaji hao ni pamoja na Kalidou Koulibaly, huku beki huyo wa Senegal, 31, akitakiwa pia na Inter Milan. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester City itapinga ofa za mkopo kwa kiungo wa kati Mwingereza James McAtee, 20, ambaye wanamtaka kuhusika kwenye kikosi chao msimu ujao. (Mail)
Chelsea wako tayari kufikia dau lolote ambalo Arsenal watawasilisha kwa Moises Caicedo wa Brighton, wakati Bayern Munich pia wanatazamia kumnunua kiungo huyo wa Ecuador, 21. (Football Insider)
Kipa wa Brentford na Uhispania David Raya, 27, amekubali masharti ya kibinafsi kuhusu kuhamia Tottenham. (Fabrizio Romano)
Nottingham Forest imekataa dau la rekodi la klabu la £30m kwa mshambuliaji wa Wales Brennan Johnson, 22, kutoka Brentford. (Sky Sports)
Burnley na Bournemouth wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure, 21, kutoka Almeria msimu huu wa joto. (Football Insider)
Newcastle imekuwa ikiwasiliana na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Desire Doue, ambaye alitimiza umri wa miaka 18 mwezi huu na amewavutia Barcelona na Paris St-Germain. (News)
Aston Villa wamekubaliana na Monchi kuondoka Sevilla na kuwa mkurugenzi wa michezo wa Villa, ambapo ataungana na meneja Unai Emery. (Football Insider)
BBC