Simba - Local

Simba yatangaza Mdhamini mpya wa jezi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jun 2023
Simba yatangaza Mdhamini mpya wa jezi

Rasmi Sandaland The Only One amesaini mkataba wa miaka miwili kutengeneza na kusambaza jezi za klabu ya Simba

Thamani ya mkataba huo ni Tsh Bilioni 2 kwa mwaka, ikiwa ni mara mbili ya pesa ambayo Vunjabei aliweka

Akizungumza katika hafla ya kumtangaza Sandaland leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah 'Try Again' amemshukuru Vunja Bei kwa udhamini wake katika miaka miwili na kumkaribisha Sandaland

"Nampongeza Sandaland kwa kupata nafasi hii, alijaribu mara ya kwanza hakufanikiwa lakini muda huu amepata. Namshukuru pia VunjaBei kwa udhamini aliotupatia," alisema Try Again

Nae Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema uongozi umefanyia kazi maoni ya Wanasimba kuhusiana na changamoto iliyojitokeza hapo awali na wana imani Mdhamini mpya Sandaland atamaliza changamoto hiyo

"Hatuwezi kuwa timu kubwa Afrika bila kuwa na uwezo wa kifedha, leo hii tunasimamia sana kwenye eneo hilo. Kwetu hatua ni safari na leo tunapiga hatua kubwa zaidi."

"Mashabiki walitwambia wanataka tuwe na jezi bora, zifike kwa wakati na zipatikane kila sehemu. Mwanzoni tulikuwa tunapata milioni 400 kwa mwaka kutokana na jezi. Akaja Vunja Bei akatupa bilioni moja kwa mwaka na huyu wa sasa anakuja kutupa bilioni mbili kwa mwaka. Namshukuru sana Sandaland kuwa mdhamini wa jezi kwa msimu wa 2023/24," alisema Kajula

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’