KMC yabaki Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th June 2023


KMC yabaki Ligi Kuu

Dakika 180 za Playoff zimeamua KMC kubaki Ligi Kuu ikishinda mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City

Mchezo wa kwanza umechezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya, Mbeya City waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na mchezo wa pili umepigwa leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salam KMC imeichapa Mbeya City 2-0

Mabao ya KMC yamefungwa dakika ya 3 na Darueshi Saliboko na dakika 28 na Aweso Aweso

Mbeya City itahitaji kushinda mchezo wa play-off dhidi ya Mashujaa ya mkoani Kigoma

Mchezo wa kwanza utapigwa Jumatatu, Juni 19 2023


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.