Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Juni 19 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Juni 19 2023

Arsenal wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 30, msimu huu wa joto kama sehemu ya marekebisho ya safu yao kati(Telegraph)

Mchezaji wa Chelsea Kai Havertz, 24, anakaribia kuhamia Arsenal , huku Bayern Munich wakiwa wamesalimisha hamu yao ya kumnunua fowadi huyo wa Ujerumani wakiwa wamechelewa. (Sky Sport Germany - in German)

Mshambulizi wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, anasema atasalia Paris St-Germain msimu ujao na kuamua mustakabali wake 2024 mkataba wake utakapokamilika.(Telefoot, via 90min)

Real Madrid wamesema watatangaza kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Joselu, 33, kutoka Espanyol wiki hii na kuondoa uwezekano wa kumnunua Mbappe msimu huu wa joto. (Sport - in Spanish)

West Ham wanaandaa ofa yao ya kwanza kwa Joao Palhinha wa Fulham huku wakimuona kiungo huyo wa kati wa Ureno, 27, kama mbadala wa Declan Rice(Fabrizio Romano)

Gianluca Scamacca amekubali masharti na Roma , huku West Ham wakiwa tayari kumruhusu mshambuliaji huyo wa Italia, 24, kuondoka kwa mkopo kisha mkataba wa kununua baada ya kipindi cha uhamisho wa mkopo.. (Football Insider)

Bayern Munich wako kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kumsajili beki wa Uingereza Kyle Walker, 33, kutoka Manchester City kwa mkataba wa kudumu (Sky Sports)

Mlinzi wa Monaco na Ufaransa Axel Disasi, 25, anasalia lengo kuu la Manchester United huku beki wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26, akitarajiwa kujiunga na Bayern kutoka Napoli . (Fabrizio Romano)

Kocha wa zamani wa Barcelona na Uhispania Luis Enrique anatarajiwa kuwa meneja mpya wa Paris St-Germain . (L'Equipe - in French)

Chelsea bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria h24, kutoka Napoli , licha ya kufikia makubaliano na Villarreal kumsajili mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 21. (90min)

Newcastle United wako tayari kuelekeza hamu yao kwa kiungo wa kati wa Nice ya Ufaransa Khephren Thuram, 22, baada ya kufadhaishwa katika harakati zao za kumtafuta kiungo wa kati wa Inter Milan wa Italia Nicolo Barella, 26. (Football Insider)

Newcastle wanaonekana kuwa tayari kutoa ofa ya kushtukiza kwa mlinda lango wa West Bromwich Albion Muingereza Josh Griffiths, 21 (Sun)

Beki wa Borussia Dortmund Mfaransa Soumaila Coulibaly, 19, yuko kwenye majadiliano ya kina kuhusu uhamisho wa mkopo kwenda Burnley (L'Equipe - in French)

Mshambulizi wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann, 32, anasema ni ndoto yake siku moja kujiunga na ligi ya Major League Soccer (Goal)

Burnley wataelekeza macho yao kwa mlinda lango wa Antwerp Mfaransa Jean Butez, 28, ikiwa watamkosa mlinda lango wa Anderlecht Mholanzi Bart Verbruggen, 20. (Sun)

Luton Town wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Morocco Ryan Mmaee, 25, kutoka Ferencvaros . (Football Insider)

PSG wanaendelea na mazungumzo na Real Mallorca kuhusu kumsajili kiungo mshambuliaji wa Korea Kusini Lee Kang-in, 22 (Marca - in Spanish)

Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji wa Brazil Vitor Roque, 18, kutoka Athletico Paranaense kwa mkataba wa miaka mitano. (Sport - in Spanish)

Baada ya kuondoka Barca msimu huu wa joto, kiungo wa zamani wa Uhispania Sergio Busquets, 34, anakaribia kusaini mkataba wa kumfuata mchezaji mwenzake wa zamani Lionel Messi kwenda Inter Miami . (Mundo Deportivo - in Spanish)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’