Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Juni 22 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Juni 22 2023

Manchester United wameungana na Arsenal kutika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24, kutoka West Ham, huku Red Devils wakizingatia mkataba wa mchezaji pamoja na pesa inayomhusisha mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 30, au kiungo wa Scotland Scott McTominay, 26. (Telegraph - usajili unahitajika)

West Ham wana nia ya kumleta McTominay kwenye klabu iwapo Rice ataondoka. (Talksport) Newcastle United wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 60 kumnunua kiungo wa AC Milan na Italia Sandro Tonali, 23. (Athletic -usajili unahitajik)

Manchester City pia wanamyatia Rice, huku West Ham wakipendelea dili ambalo lingemfanya kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, kuhamia London Stadium. (ESPN)

Kiungo wa kati wa City na Ureno Bernardo Silva, 28, anakaribia kuhamia Saudi Arabia. (Marca kwa Kihispania)

Bayern Munich wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 31, kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto, huku Newcastle ikimtaka. (Bild - kwa Kijerumani)

The Magpies pia wanataka kumsajili Ruben Neves, 26, kwa mkopo baada ya kiungo huyo wa Ureno kukubali kujiunga na Al Hilal kutoka Wolverhampton Wanderers kwa £47m wiki hii. (Football Insider)

Mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, bado ana matumaini ya kuhamia Manchester United msimu huu wa joto. (Mirror)

Spurs wamekubali mkataba wa pauni milioni 17.2 kumsaini kipa wa Italia Guglielmo Vicario, 26, kutoka Empoli. (Sky Sports)

Manchester United na Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa Randal Kolo Muani, 24. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

The Red Devils wanafikiria kumnunua kipa wa Inter Milan wa Cameroon, Andre Onana, 27. (Sky Sports Italy - kwa Kitaliano)

Burnley wanatazamiwa kumsajili beki wa Jamhuri ya Ireland Dara O'Shea, 24, kutoka West Bromwich Albion. (Irish independent)

Bournemouth wanakaribia kukamilisha dili la £9.5m na Roma kwa ajili ya kumnunua mshambulizi wa Uholanzi Justin Kluivert, 24. (Talksport)

Brentford wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili beki wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, 22, kutoka Wolves. (Sky Sports)

Kiungo wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 21, amesema huenda akalazimika kuhama ili kupata muda zaidi wa kucheza, na yuko tayari kujiunga na Liverpool. (Mirror)

Juventus wamempa kiungo wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, mkataba mpya kabla ya mkataba wakewa sasa kukamilika mwezi Julai, lakini angependelea kuhama Ligi ya Premia, huku Manchester United na Newcastle zikivutiwa. (Foot Mercado - Kwa Kifaransa)

Kiungo wa Italia Jorginho, 31, anataka kusalia Arsenal licha ya Lazio kuonyesha nia ya kuta kumsajili. (Evening Standard) Kiungo wa kati wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 30, anakaribia kuhamia Al-Nassr kwa pauni milioni nane. (Standard)

Kiungo mwenza wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 22, pia anaweza kuondoka kuelekea Saudi Arabia huku klabu mbili za Pro League zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
35m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
47m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’