Baada ya miaka 13 Simba jana Simba iliagana na kiungo Jonas Mkude. Mkude anaingia kwenye msululu wa wachezaji wa Simba ambao wamekumbana na Thank You kutoka klabu ya Simba
Simba ilitangaza kuachana na wachezaji wengine wawili, mlinda lango Beno Kakolanya na kiraka Eraston nyoni
Mpaka sasa Simba imetangaza kuachana na wachezaji saba ambao ni Augustine Okrah, Mohamed Ouattara, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Nelson Okwa, Victor Akpan na Jonas Mkude
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amesema wamejipanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao ili kwendana na malengo waliyojiwekea kuelekea msimu wa 2023/24