Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Juni 23 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Juni 23 2023

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, 31, ndiye mchezaji mwingine anayesakwa na Saudi Pro League baada ya kuwasili kwa Karim Benzema na N'Golo Kante. (Four Four Two)

Wakala wa Jurgen Klopp amepuuzilia mbali tetesi kwamba kocha huyo mkuu wa Liverpool anaondoka Anfield kwenda kuchukua mikoba ya Hansi Flick kama kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani. (Mirror)

AC Milan wanatumai kuwashinda mahasimu wao Inter Milan katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku, 30, (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Manchester United wameafikiana na Chelsea kuhusu dili la la kumsajili kiungo wa Uingereza Mason Mount, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akikaribia kununuliwa kwa pauni milioni 60. (Mirror)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anaamini kuwa kiungo wa Uingereza Declan Rice, 24, ndiye nahodha wa baadaye wa klabu hiyo na The Gunners wanajiandaa kuwasilisha ofa ya tatu hivi karibuni na mahitaji mengine ya West Ham. (Mail)

Rice bado ana nia ya kujiunga na Arsenal licha ya Manchester City kuonyesha nia ya kujiunga na kinyang'anyiro hicho na washindi wa Treble pia kuweza kukidhi bei ya £100m. (Guardian)

Tottenham wameibuka kuwa mstari wa mbele kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 26. (Guardian)

Bayern Munich wako tayari kumpa mkataba wa miaka miwili beki wa kulia wa Manchester City na Uingereza Kyle Walker, 33. (Bild - Kwa Kijerumani)

Fulham wanaongoza kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa Southampton na England James Ward-Prowse, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa tayari kuhamia Craven Cottage baada ya Saints kushushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Independent)

Borussia Dortmund wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 13 kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Tunisia Hannibal Mejbri, 20, ambaye msimu uliopita alichezea Birmingham kwa mkopo . (Manchester Evening News)

Klabu hiyo ya Bundesliga pia inamtaka kiungo wa kati wa Manchester City Cole Palmer, 21, huku Dortmund wakitafuta mbadala wa Jude Bellingham. (Bild - kwa Kijerumani)

Manchester United imeipatia Roma nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26. (Metro)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
5h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
9h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
13h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
13h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
15h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
16h ago
READ MORE β†’