Mrithi wa Nasreddine Nabi ni Miguel Gamondi raia wa Algentina, klabu ya Yanga imemtangaza leo katika Mkutano Mkuu wa Wanachama
Gamondi anatua Yanga akiwa na uzoefu mkubwa katika soka la Afrika
Amewahi kuzifundisha Wydad Athletic, Esperance, Asec Mimosas na Mamelodi Sundowns
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Yanga imeweka malengo makubwa msimu ujao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika