Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Juni 26 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Jun 2023
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Juni 26 2023

Manchester City wamewasilisha dau la euro 90m (£77m) kwa Josko Gvardiol wa RB Leipzig, 21, huku beki huyo wa Croatia akitajwa kama "mchezaji ndoto" wa Pep Guardiola. (Sky Sport Ujerumani – In Germany )

Mshambulizi wa Villarreal na Senegal Nicolas Jackson, 22, anatazamiwa kukamilisha uhamisho wa euro 35m (£30m) kwenda Chelsea baada ya kukamilisha uchunguzi wa afya katika klabu hiyo Jumapili. (Subscription Required )

Mikel Arteta anasema anafuraha Arsenal na amepuuza ripoti zinazomhusisha na Paris St-Germain. (Marca in Spanish)

Klabu ya Saudi Pro League, Al-Hilal inataka kumsajili winga wa Jamaica Demarai Gray, 26, kutoka Everton, huku mazungumzo yakipangwa kufanyika wiki ijayo. (Mail)

Beki wa kati wa Colombia Yerry Mina, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Everton mwishoni mwa msimu huu, anatarajiwa kusajiliwa na Fulham. (Sun)

Al-Nassr wanatumai kukamilisha dili la winga wa Chelsea kutoka Morocco Hakim Ziyech, 30, mapema wiki hii, na kumfanya kuwa mchezaji wa nne kuondoka Stamford Bridge kwenda Saudi Arabia msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ataruhusu wachezaji 11 kuondoka Old Trafford msimu huu wa joto huku akiomba kuchangisha zaidi ya pauni milioni 100 kusaidia kubadilisha kikosi chake. (Sun)

United inamtazama kiungo wa kati wa Ajax na Ghana Mohammed Kudus, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Utrecht wa Marekani Taylor Booth, 22, baada ya kushindwa kufanya maendeleo na Chelsea kuhusu mpango wa kumnunua Mason Mount. (ESPN)

Mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel anatamani kuungana tena na kiungo wa kati wa Uingereza Mount, 24, ambaye alikuwa akimfundisha Stamford Bridge. (Guardian)

Liverpool wanajipanga kushindana na Tottenham kumnunua mlinzi wa Uholanzi Micky van de Ven, 22, ambaye yuko tayari kuondoka Wolfsburg msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uturuki Arda Guler, 18, anavutiwa na Arsenal, Liverpool, Real Madrid na Benfica baada ya kuvutiwa na Fenerbahce. (Record – in Poruguese )

Gerardo 'Tata' Martino, ambaye amewahi kumfundisha Lionel Messi huko Barcelona na Argentina, anaweza kuwa kocha wake kwa mara ya tatu baada ya kufanya mazungumzo ya kuchukua mikoba ya kumfunza mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 36 katika klabu mpya ya Inter Miami. (Subscription Required)

Fulham wamefanya mpango wa kumsajili fowadi wa Marekani Brenden Aaronson, 22, kwa mkopo kutoka Leeds United. (Mail)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
48m ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
2h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
3h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
9h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
10h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’