Yanga - Local - Transfer

Yanga yatajwa kumuwania Mkude

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Jun 2023
Yanga yatajwa kumuwania Mkude

Zinavuna kila kona tetesi kuhusu kiungo Jonas Mkude ambaye hataendea kuitumikia klabu ya Simba baada ya mkataba wake kumalizika na timu hiyo kutangaza kuachana nae

Zipo taarifa za ndani kuwa mabosi wa Yanga wanaweza kumpa Mkude mkataba wa mwaka mmoja wakiamini anaweza kuongeza kitu katika kikosi cha Yanga

Mkude ni miongoni mwa viungo bora walioyajenga majina yao katika soka la Tanzania kwa muda mrefu

Yawezekana kwa sasa sio yule Mkude wa misimu kadhaa iliyopita lakini bado ni mchezaji anayeweza kuongezea timu hiyo ubora katika eneo la kiungo

Hata hivyo huku Yanga eneo la kiungo tayari lina Yannick Bangala, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Salum Abubakar na Zawadi Mauya huku Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe akitamba kuna namba 6 mwingine matata atatambulishwa wiki ijayo

Ni wazi kama Yanga itamsajili Mkude atakuwa na kazi ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo

Mkude alipata mafanikio makubwa wakati akiwa Simba, kabla ya msimu uliopita, alikuwa na uhakika wa kupata nafasi ya kucheza karibu kila mechi katika kikosi kilichokuwa kimesheheni wachezaji bora

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
24m ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
4h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
5h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
6h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
7h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
7h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’