Licha ya kurejeshwa na kufanya mazoezi katika kikosi cha Simba mwishoni mwa msimu uliopita, kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga amejiunga na JKT Tanzania
Dilunga alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alipendekeza wasajiliwe na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao
Hata hivyo ofa nono ya JKT Tanzania imemshawishi Dilunga kuwakacha wekundu hao wa Msimbazi na kuibukia kwa maafande
Dilunga alikuwa nje msimu mzima uliopita akiuguza majeraha ambayo alipata wakati akiitumikia Simba mwishoni mwa msimu wa 2021/22
Baada ya kurejea kwenye Ligi Kuu, JKT Tanzania inajiimarisha ili kuhakikisha inaleta ushindani