Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Julai 02 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Julai 02 2023

Dau la Manchester United la pauni milioni 30 kwa ajili ya mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20, limekataliwa. (Corriere dello sport, in Italian)

Mkurugenzi Mtendaji wa Inter Milan Beppe Marotta amethibitisha nia ya Manchester United ya kutaka kumsajili kipa wa klabu hiyo ya Italia na Cameroon Andre Onana, 27. (Mail)

United pia wanavutiwa na kipa wa Feyenoord, Mholanzi, Justin Bijlow, 25, kama mchezaji wao mwingine endapo watamkosa Onana. (Mirror)

Mkataba wa Newcastle kumsajili kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali, 23, kutoka AC Milan unatazamiwa kukamilika lakini unaweza kucheleweshwa hadi wiki ijayo. (Fabrizio Romano)

Real Madrid wanatumai kushindana na Barcelona katika jitihada za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Fenerbahce Arda Guler. Mchezaji huyo wa Uturuki mwenye umri wa miaka 18 ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 15 katika kandarasi yake, ambayo itakamilika 2025. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

West Ham wamemuondoa Declan Rice kama chaguo ambalo mashabiki wanaweza kubinafsisha jezi zao huku mazungumzo ya uhamisho wa pauni milioni 105 na Arsenal kumnunua kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 24 unakaribia mwisho. (Mirror)

Mlinzi wa Chelsea Mwingereza mwenye umri wa miaka 20 Levi Colwill anatarajiwa kuwa na jukumu muhimu chini ya meneja mpya Mauricio Pochettino huku Brighton, Liverpool na Manchester City zikionesha nia ya kumsaka. (Football.London)

Kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Juan Mata, 35, ametangaza kuondoka Galatasaray ya Uturuki. (Tribal Football)

Mlinzi wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 22, atakamilisha uhamisho wa kwenda Arsenal wenye thamani ya £45m wiki hii. (Mirror)

Mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz, 24, amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal kwa £17m kwa mwaka baada ya kujiunga kutoka kwa wapinzani wa London Chelsea. (Bild, via Goal)

Kiungo wa kati wa Uingereza Danny Drinkwater, 33, anasema angependa kujiunga tena na Leicester City baada ya kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Chelsea mwaka wa 2017. (SportBible)

Haiwezekani Manchester United kumsajili kiungo wa Austria Marcel Sabitzer, 29, au 30- Mchezaji wa zamani wa Uholanzi Wout Weghorst kwa mkataba wa kudumu baada ya mikataba yao ya mkopo kukamilika Ijumaa. (Manchester Evening News)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
5h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
9h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
12h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
13h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
14h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
14h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
15h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
16h ago
READ MORE β†’