Yanga - Local

Mayele awashukia wanaotaka aondoke Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Jul 2023
Mayele awashukia wanaotaka aondoke Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameeleza kushangazwa na watu wanaotaka aondoke kwenda timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo

Mayele ametoa kauli hiyo baada ya kuzisikia kauli za baadhi ya mashabiki hasa wa upande wa pili na wachambuzi ambao kila kukicha wanaibua tetesi za yeye kuondoka Yanga huku wengine wakimshauri aondoke

"Wakati nakuja hapa Tanzania hakuna mtu aliyenijua, nilichokifanya ni kujituma na nidhamu. Ninaipenda kazi yangu ndio maana leo kila mtu anamuimba Mayele"

"Nilisema tangu nikiwa mdogo malengo yangu ni kucheza mpira na nitafanikiwa kupitia soka, kwa sasa naona nimeanza kutimiza malengo yangu na kupata japo mafanikio lakini sijafikia hata nusu ya malengo yangu, nitaendelea kupambana zaidi"

"Ninawashangaa wanaotaka niondoke Yanga, watu wanasubiri kwa hamu 'Thank You' ya Mayele, mimi bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Yanga na ninaheshimu mkataba wangu, ikija ofa tutakaa mezani tutazungumza,” amesema Mayele

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema jukumu la uongozi wake ni kuhakikisha wanawabakisha wachezaji wote muhimu kikosini

Tayari Yanga wamempa Mayele ofa ya mkataba mpya kukiwa na maboresho ya mshahara wake 

Hata hivyo Yanga imeweka wazi msimamo wake kuwa iko tayari kuzingatia maamuzi yenye maslahi kwa pande zote mbili ikitokea kuna timu imewasilisha ofa nono zaidi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’