Bayern Munich wanapanga kuwasilisha ofa ya pili kwa klabu ya Tottenham kwa lengo la kumnunua mshambuliaji wao wa Uingereza Harry Kane, 29. (Sky Sport - kwa Kijerumani)
Manchester City wanatayarisha ofa yao ya kwanza kumnunua mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 21, baada ya kuanza mazungumzo na RB Leipzig. (ESPN)
Kiungo wa Liverpool na Uingereza Jordan Henderson, 33, na mshambuliaji wa Chelsea na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 34, ni wachezaji wawili wanaoweza kusajiliwa na Al-Ettifaq baada ya klabu hiyo ya Saudia kumteua Steven Gerrard kama mkufunzi wao mpya. (Mail)
Paris St-Germain wanapaniaa kuzishinda Chelsea, Liverpool na Manchester City katika mbio za usajili kiungo wa Uhispania Gabri Veiga, 21, kutoka Celta Vigo. (Guardian)
Chelsea wamefanya mazungumzo na Southampton kuhusu uwezekano wa kumnunua beki wao wa zamani Tino Livramento, 20. Southampton wanamthamini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 21, ambaye pia anawindwa na Newcastle, kwa pauni milioni 38. (Mail)
Liverpool wamepiga hatua mbele ya Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia na wanaandaa ofa ya ufunguzi kwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye Southampton wanasema ni ya thamani ya £50m. (talkSPORT)
Al-Nassr wametoa ofa nono kwa kipa wa Cameroon na Inter Milan Andre Onana, 27, ambaye pia analengwa na Manchester United. (CBS)
Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 30, atakamilisha uhamisho wa pauni milioni 21.5 kwenda Bayer Leverkusen wiki hii. (Sun)
Everton wameiambia Almeria kwamba wana nia ya kufikia kipengele cha kuachiliwa kwa El Bilal Toure cha euro milioni 40, ingawa Fulham wanaweza kumnunua mshambulizi huyo wa Mali, 21, ikiwa watamuuza mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 28, msimu huu wa joto. (Sacha Tavolieri)
Christian Pulisic wa Chelsea hana nia ya kuhamia Lyon msimu huu wa joto kwani winga huyo wa Marekani, 24, anapendelea kujiunga na AC Milan baada ya kuafikiana kimsingi na klabu hiyo ya Serie A. (ESPN)
Newcastle wanatafakari uwezekano wa kumnunua beki wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, 21. (Football Insider) Brighton wana nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 22, kutoka Ajax. (Athletic, usajili unahitajika)
Wolves wako tayari kumuuza beki Mwingereza Max Kilman mwenye umri wa miaka 26 msimu huu wa joto, licha ya kukataa ofa kutoka kwa Napoli. (90 min)
Chelsea wanataka kumuuza Callum Hudson-Odoi msimu huu wa joto, huku Nottingham Forest ikiwa miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili winga huyo wa Uingereza, 22. (Football Transfers)
Manchester City wako tayari kulipa Atletico Madrid euro 15m (£12.9m) kwa ajili ya winga wa Uhispania Rodrigo Riquelme, 23, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu dada ya City Girona. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Leicester City wanatafuta kumnunua beki wa Manchester City Muingereza Callum Doyle, 19. (Athletic, usajili unahitajika)
Bordeaux wanatarajia Josh Maja kuondoka katika klabu hiyo kwani mshambuliaji huyo mzaliwa wa Uingereza, 24, sasa ni mchezaji huru na hajajibu ofa ya kuongezewa mwaka mmoja. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
BBC