Manchester City wako tayari kukubali dau la kati ya £45 na £50m msimu huu wa joto kwa ajili ya winga wa Ureno Bernardo Silva, 28. (Football Insider)
Newcastle United wana nia ya kutaka kumnunua beki wa England Marc Guehi, 22, ingawa Crystal Palace inaomba ada ya takriban £60m. (Football Insider)
Thiago Alcantara anavutia vilabu vya kigeni, zikiwemo za Saudi Arabia, ingawa Liverpool bado hawajapokea ofa rasmi ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uhispania, 32. (Times - usajili unahitajika)
Barcelona wamekubali dili la kumsajili Vitor Roque kutoka Athletico Paranaense lakini lazima waone kama wanaweza kupunguza bili yao ya mshahara kabla ya kujua kama mshambulizi huyo wa Brazil, 18, anaweza kujiunga naq msimu huu wa joto, Januari au msimu ujao wa joto. (Sport - kwa Kihispania)
Arsenal, Manchester City, Manchester United na Tottenham ni miongoni mwa klabu kubwa ambazo zimeonyesha nia ya kumnunua kiungo wa Red Bull Salzburg Israel Oscar Gloukh, 19. (Guardian).
Kipa wa Brighton wa Uhispania Robert Sanchez, 25, ameibuka kama shabaha inayolengwa na Manchester United. (Mail)
Mpango wa Arsenal wa kumsaini kiungo wa Uingereza na West Ham Declan Rice, 24 kwa mkataba wa pauni milioni 105, unakaribia kukamilika, huku sehemu ya ada hiyo ikitarajiwa kulipwa kwa awamu tatu. (Guardian)
Barca wameitangulia Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kumnunua Arda Guler wa Uturuki kutoka Fenerbahce, huku AC Milan na Borussia Dortmund wakiachana na harakati zao za kumnasa kiungo huyo mshambuliaji, 18. (Sport - kwa Kihispania)
Guler pia amepokea ofa kutoka kwa Arsenal na Sevilla lakini angependelea kujiunga na Real Madrid. (AS - kwa Kihispania)
Real wameitaka Inter Milan kutaja bei ya kumnunua mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 25. (Sport - kwa Kihispania)
Brighton wameongeza juhudi yao ya kumnunua beki wa Ajax na Nigeria Calvin Bassey, 23, kama mbadala wa mlinzi wa Chelsea Muingereza Levi Colwill, 20. (The Athletic - usajili unahitajika )
Almeria wanasema Everton na vilabu viwili vya Italia vimewasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Mali El Bilal Toure, 21. (Diario de Almeria - kwa Kihispania)
Winga wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 22, ameamua kuondoka Chelsea msimu huu wa joto, huku AC Milan ikiingia kwenye mbio za kumsajili. (Metro) Tino Livramento wa Southampton angependelea kuhamia Newcastle baada ya Chelsea kuonyesha nia ya kumnunua tena beki huyo wa Uingereza, 20. (Mail)
Arsenal wako tayari kumuuza Folarin Balogun msimu huu wa joto na wameweka thamani ya £50m kwa mshambuliaji huyo wa Marekani, 22. (Mirror).
Arsenal wanatazamiwa kukubaliana kuongeza mkataba na beki wa Ufaransa William Saliba, 22, ambao utadumu hadi 2027. (Fabrizio Romano).
Lakini kiungo wa kati wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 23, amesema anataka kuondoka Arsenal msimu huu wa joto. (Mirror)
Manchester United wamepewa nafasi ya kuchuana na Atletico Madrid kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Fiorentina kutoka Morocco Sofyan Amrabat, 26. (90min).
Winga wa Newcastle Mfaransa Allan Saint-Maximin, 26, ameibuka kama mchezaji wa hivi punde zaidi wa Ligi Kuu ya Uingereza kulengwa na Saudi Pro League. (90min)
Aaron Ramsey amefanya mazungumzo na Cardiff kuhusu mpango wa kurejea katika klabu yake ya utotoni baada ya kiungo huyo wa Wales, 32, kuachiliwa na klabu ya Nice ya Ufaransa. (Talksport)
BBC



