Hatimaye ule wakati wa mashabiki wa Simba kuwafahamu wachezaji wao waliosajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu yao umewadia
Leo saa 7 mchana Simba itamtambulisha mchezaji wa kwanza aliyetua kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika mashindano mbalimbali 2023/24
"Muda wa kusubiri umekwisha kesho (leo) saa 7:00 mchana tutaanza kushusha watu wa kazi!," ujumbe wa Simba ulibainisha
Miongoni mwa wachezaji wanaosubiri utambulisho ni kiungo Fabrice Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan
Simba inadaiwa kuwazidi ujanja watani zao Yanga kwenye usajili wa kiungo uyo ambaye huvaa jezi namba sita