Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Julai 07 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Julai 07 2023

Manchester United wanakaribia kumsajili kipa wa Inter Andre Onana, 27, baada ya kuafikiana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon. (Fabrizio Romano)

The Red Devils pia wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20 kwa pauni milioni 50. (Telegraph)

Chelsea italazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 100 ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, msimu huu wa joto (Telegraph)

Newcastle wanajiandaa kumnunua beki mkongwe wa Italia na Juventus Leonardo Bonucci, 36, ili kuongeza uzoefu katika kampeni yao ijayo ya Ligi ya Mabingwa. (TEAMtalk)

Jurrien Timber wa Ajax atafanyiwa vipimo vya afya Arsenal siku ya Ijumaa huku The Gunners wakiwa na uhakika wa kukamilisha dili la pauni milioni 38.5 kwa ajili ya beki huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22. (Standard)

Kiungo wa Tottenham Ivan Perisic amemwambia mkufunzi Ange Postecoglou kwamba ana nia ya kusitisha mkataba wake, huku Mcroatia huyo mwenye umri wa miaka 34 akitaka kujiunga na Hajduk Split. (Gianluca Di Marzio)

Wakati huo huo, Atletico Madrid wamewasiliana na kiungo wa Spurs na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, ambaye pia amekuwa akihusishwa na uhamisho wa Bayern Munich. (Mail)

Southampton wanaamini kuwa watapewa bei inayotakiwa ya pauni milioni 50 wanapojiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, huku Chelsea, Liverpool na Arsenal pia wakiwania saini yake. (Sky Sports)

Matumaini ya Crystal Palace kumnunua tena Wilfried Zaha, 30, yamefifia huku mshambuliaji huyo akizingatia ofa kutoka kwa Lazio, Fenerbahce na Al-Nassr. (Standard)

Fulham wanakaribia kufikia mkataba mpya na mchezaji huru Willian baada ya mshambulizi huyo wa Brazil, 34, kuwa mchezaji huru mwishoni mwa juma lililopita. (The Athletic - usajili unahitajika)

Beki wa Arsenal Mfaransa William Saliba, 22, ametia saini mkataba mpya utakaomweka Emirates Stadium hadi 2027. (The Athletic - usajili unahitajika)

West Ham wanafikiria kumsajili kiungo wa Juventus Denis Zakaria. The Hammers kwanza wanaweza kumchukua kwa mkopo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 26 na chaguo la kumnunua kwa £15.4m. (Standard)

The Hammers pia wanavutiwa na wachezaji wa Joao Palhinha, 27, wa Fulham na James Ward-Prowse wa Southampton mwenye umri wa miaka 28 wanapokiandaa kuimarisha kikosi chao . (Guardian)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
9h ago
READ MORE β†’
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
9h ago
READ MORE β†’
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
13h ago
READ MORE β†’
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
16h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
17h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
17h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
18h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
19h ago
READ MORE β†’