Jana klabu ya Chelsea ilimuaga nahodha wake Cesar Azpilicueta baada ya takribani miaka 11 darajani
Mwenyekiti wa Chelsea, Toddy Boehly na mmiliki wa Behdad Eghbali wamesema kuondoka kwa Cesar ni heshima kwa klabu hiyo
Azpilicueta ameondoka kama mshindi na mchezaji mwenye heshima kubwa. Mhispania huyo ameripotiwa kuwa huenda akajiunga na Atletico Madrid baada ya kukubali mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru
Taarifa ya Chelsea pia imempongeza beki huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Marseille ya Ufaransa. Akiwa Chelsea Cesar amecheza michezo 508, ameshinda mataji tisa, amecheza chini ya makocha tisa tofauti akiwa Stanford