Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Julai 08 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Julai 08 2023

Newcastle United wanatumai kuwa wanaweza kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 35 kwa winga wa Leicester City Harvey Barnes ili kuzipiku Aston Villa na West Ham kuipatasaini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Guardian)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe anafikiria kuwa huenda akalazimika kuondoka Paris St-Germain msimu huu wa joto kwani bado hana mpango wa kuongeza mkataba wake zaidi ya mwaka 2024 na chaguo la timu ambayo anapenda kujiunga nayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ni Real Madrid. (ESPN)

PSG wanaamini Mbappe tayari amekubali kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao wa joto na, ikiwa hatasaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Ufaransa, watamuuza kwa dau la juu zaidi msimu huu wa joto bila kujali ni nani. (Sky Sports)

Chaguo la kwanza la Mbappe ikiwa angehamia Ligi ya Premia litakuwa ni Arsenal lakini yuko nje ya bajeti ya The Gunners na hakuna mawasiliano yaliyofanywa kati ya pande hizo mbili. (Independent)

Mshambuliaji wa Ureno Joao Felix anataka kuhamia PSG lakini anaweza kuishia kusalia Atletico Madrid, ambao wanataka euro 100m kwa mchezaji huyo wa miaka 23. (AS – in Spanish)

Inter Milan wanaongeza bidhii katika kumsaka mlinda mlango wa Tottenham Hugo Lloris, 36, huku wakipanga Mfaransa huyo achukue nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana, 27, ambaye analengwa na Manchester United. (Foot Mercato - in French)

Sporting Lisbon wamekubali mkataba wenye thamani ya euro 24m (£20.5m) na Coventry City kwa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 25. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone anakaribia kukataa ofa nono kwa meneja wa klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia ili kusalia na timu hiyo ya Uhispania. (ESPN)

Hatua ya Mason Greenwood ya uhamisho katika wa kutoka katika kandanda kwa miezi 18 unaweza kukamilika, huku Atalanta akitaka kumnunua mshambuliaji huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka 21 kwa mkopo. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amerejea mazoezini na Everton huku akilenga kurudisha kazi yake kwenye mstari, ambapo mkufunzi wa Toffees Sean Dyche amemwambia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuwa anahitaji "kujiweka sawa". (Mail)

Chama cha Soka kitampa Lee Carsley kandarasi mpya ya kusalia kama meneja wa England chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuiongoza timu hiyo kutinga fainali ya Uefa Championi ya vijana wenye chini ya miaka 21. (Mail)

Beki wa zamani wa Chelsea John Terry anasema amerejea katika klabu hiyo ya Stamford Bridge na "anafanya kazi katika shule ya soka". (John Terry)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’