Manchester United wameweka thamani inayotakiwa ya £50m kwa klabu inayotaka kumnunua beki wa England Harry Maguire, 30. (Manchester Evening News)
West Ham wanatumai kumnunua kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 28, kwa ada ya £20m lakini Southampton wanataka karibu £40m kwa ajili ya nahodha wao huyo (Mail)
Wolves wanakaribia kumsajili tena beki wa pembeni wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 31, baada ya kuondoka Atletico Madrid. (TeamTalk)
Uhamisho wa kipa wa Cameroon Andre Onana wa pauni milioni 43 kutoka Inter Milan kwenda Manchester United uko katika hatua za mwisho na utakamilika wiki hii baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kukubaliana maslahi binafsi. (Mail)
Donny van de Beek, 26, pia anaweza kuwa njiani kuondoka Manchester United msimu huu wa joto huku Nottingham Forest, Wolves na Crystal Palace wakimtaka kiungo huyo wa kati wa Uholanzi. (90Min)
Tottenham Hotspur wana uhakika wa kumsajili beki wa Wolfsburg Mholanzi Micky van de Ven, 22, ambaye thamani yake ni pauni milioni 25. (Mirror)
Everton wamefanya uchunguzi kuhusu kumsajili mlinda mlango wa zamani wa Manchester United Tom Heaton, 37. (Mirror)
Mshambulizi wa Montpellier Mfaransa Elye Wahi, 20, na mshambuliaji wa Juventus raia wa Serbia Dusan Vlahovic, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaosakwa na Chelsea. (Evening Standard)
Beki wa kati wa Torino Mholanzi Perr Schuurs, 23, anafukuziwa na Liverpool huku kocha Jurgen Klopp akijaribu kuimarisha safu yake ya ulinzi bila kutumia ada kubwa. (Football Insider)
Newcastle United inaweza kumuuza winga Mfaransa mwenye umri wa miaka 26 Allan Saint-Maximin - ambaye anasakwa na baadhi ya vilabu vya Saudia - kusaidia kupata fedha za kumnunu Muingereza wa Leicester City Harvey Barnes, 25. (Telegraph)
Leicester City wana nia ya kumsajili mshambuliaji Muingereza Stephy Mavididi, 25, kutoka Montpellier. (Fabrizio Romano)
Inter Milan wanajiandaa kuongeza dau lao la kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, kutoka kwa ofa yao ya awali ya pauni milioni 23 - lakini The Blues wanataka pauni milioni 40. (Times)
Al-Hilal wameifahamisha Manchester City kwamba wako tayari kulipa pauni milioni 60 kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva. (CBS Sports)
Beki wa kulia wa Uingereza Reece James, 23, anataka kuwa nahodha mpya wa Chelsea - licha ya kutakiwa Real Madrid. (Podcast via Mirror)
Sheffield Wednesday wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Uingereza Troy Deeney mwenye umri wa miaka 35 kuhusu nafasi ya kocha mchezaji. (Mail)
Kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 28 atajiunga na Al-Hilal ya Saudi Arabia kutoka Lazio kwa uhamisho wa thamani ya £34m. (Gola)
Paris St-Germain sasa wanaongoza mbio za kumnasa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa Randal Kolo Muani, 24. (Independent)
Luton Town wanamtaka mlinda mlango wa Blackburn Rovers raia wa Ubelgiji Thomas Kaminski, 30, lakini bado hawajafikia kati ya pauni milioni 3-4 zinazotakiwa. (Lancashire Telegraph)
BBC



